BIBLIA YASEMA
Would you like to react to this message? Create an account in a few clicks or log in to continue.

Go down
avatar
Admin
Admin
Posts : 8
Join date : 2018-02-03
https://biblia-yasema.board-directory.net

Mwongozo,jumatatu tar 5/2 Empty Mwongozo,jumatatu tar 5/2

Mon Feb 05, 2018 3:59 pm
Utiifu


Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili; kwa maana atamchukia huyu, na kumpenda huyu; ama atashikamana na huyu, na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali.” (Mathayo 6:24). Aya hii hutufundisha nini kuhusu umuhimu wa juu kabisa wa utii kwa Mungu?

Kufahamu ya kuwa jina la Mungu humaanisha “mwenye wivu” (Kutoka 34:14) kungepasa kutupatia wito ulio wazi wa utiifu. Utii kwa Mungu “mwenye wivu” ni utii katika upendo. Katika vita vya imani, utii husaidia kufafanua ya kuwa sisi tu akina nani na kututia moyo kudumu katika mapambano. Utii wetu ni muhimu kwa Mungu (1 Wafalme 8:61). Sio mkataba unaojaribu kutabiri kila dharura; wala sio tu orodha ya kanuni. Badala yake, ni udhihirisho unaoonekana wa mawazo binafsi, imani, na msimamo.


Soma 1 Mambo ya Nyakati 28:9. Andiko hili linatufundisha nini kuhusu umuhimu wa utii?

Mahali ambapo pana utii, hata hivyo, pana uwezekano wa usaliti. Utii, ni kama upendo, ni lazima utolewe kwa uhuru, ama sivyo sio utii wa kweli. Katika vita, nyakati zingine majeshi ya msitari wa mbele wanalazimika kusimama na kuendelea kupigana; vinginevyo, mkuu wao angeliamuru wapigwe risasi. Watu kama hawa wangeliweza kutekeleza wajibu wao, lakini kimsingi itakuwa sio kwa utii. Huo sio aina ya utii ambao Mungu anautaka kutoka kwetu.

Mwangalie Ayubu. Hakuwa amejua matukio ya misiba iliyokuwa inakuja mbele kuangamiza familia, mali, na afya yake. Angelikoma kuamini, kupenda, na kuwa na msimamo, lakini utii wake kwa Mungu ulikuwa ni uchaguzi usioyumba wa uadilifu. Mwaminifu na asiyeogopa kumsifu Mungu hadharani, alitamka maneno maarufu “Tazama, ataniua; sina tumaini; ila hata hivyo nitaithibitisha njia yangu mbele yake.” (Ayubu 13:15). Uaminifu wake mbele ya msiba ndio kiini cha utii, na unawaeleza mawakili waaminifu katika ubora wao wa juu kabisa.


Jiulize mwenyewe: Mimi ni mwaminifu kiasi gani kwa Bwana, aliyenifia? Ni kwa njia zipi ningeliweza kuudhihirisha utii huo kwa uzuri zaidi?



Karibu sana
Back to top
Permissions in this forum:
You cannot reply to topics in this forum